Ndugu msomaji, na ieleweke kuwa, kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake.
Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary), hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kitaalam kama ‘Ovaritis.’
Vyanzo Vyake
Visababishi vya tatizo la kuvimbe kwa mayai ya mwanamke ni kama ifuatavyo;
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
- Kufanya tendo la ndoa wakati mwanamke akiwa hedhini.
- Kuwa na mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum
- Kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili, na hii ni kwa wale wanawake wanene.
- Ugumba na kuvunja ungo au kubalehe mapema hasa miaka 11 au chini ya hapo,
- Kukosekana uwiano sawa wa vichocheo au homoni mwilini au ugonjwa wa hypothyroidism.
- Utoaji mimba
Dalili Zake.
Kwa kawaida uvimbe katika mayai huonyesha dalili zifuatazo:
- Maumivu makali, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, ambapo maumivu hayo yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja. Pia mtu anaweza kupata usumbufu na kutojisikia vizuri kwenye maeneo ya chini ya kitovu, kwenye nyonga, uke, kwenye mapaja na mgongoni upande wa
- Kuhisi tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba.
- Maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum.
- Maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati wa hedhi na ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya chini mgongoni. Maumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
- Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya kujamiiana. Kuhisi kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni.
- Ugumba na kuhisi uchovu, mabadiliko ya haja ndogo yaani kukojoa mara kwa mara, kujikojolea au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo. Vilevile mabadiliko ya haja kubwa ambayo ni kupata haja kubwa kwa shida sana kutokana na presha kwenye maeneo ya nyonga.
- Nywele kukua kwa kasi na kuongezeka kuota kwa nywele kwenye uso au sehemu nyingine za mwili.
- Kichwa kuuma, kuongezeka uzito, maumivu kwenye mbavu, kutokewa na uvimbe chini ya ngozi na kuvimba mara kwa mara.
Vipimo Vya Uchunguzi:
Kwanza kabisa mgonjwa anapaswa kufanyiwa Endovaginal Ultrasound ambayo hufanywa kwa kuingiza mpira maalum kupitia ukeni na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua kama uvimbe kwenye mayai ni wa aina gani na kujua kama ni maji tu (fluid filled sac), au ni maji pamoja na mchanganyiko wa vitu vigumu kwa maana ya complex, au ni vitu vigumu pekee ambapo huitwa completely solid.
Kipimo kingine kinachochukuliwa kuchunguza ugonjwa huu ni Abdominal Pelvic Ultrasound ambayo ni Ultrasound ya kawaida. Husaidia kujua ni aina gani ya uvimbe uliopo kwenye mayai ya mwanamke.
Wapendwa wasikilizaji, napenda kuwashauri wale wote wanaosumbuliwa na matatizo haya ya uvimbe wa mayai kwenda kupata vipimo vya Ultrasound ili kuhakikisha uvimbe una ukubwa gani, na kisha njoo upate dawa za asili katika JAMES HERBAL CLINIC ambazo tumeziandaa kwa ajili ya kuondoa uvimbe unaokusumbua.
Kwa mawasiliano nipigie: 0752389252 au 0712181626