Kwanini Mirija Ya Uzazi Huvimba?

Kitaalamu kuvimba kwa mirija ya uzazi tunaita “Salpingitis”. Hii huwa ni hali ya maambukizi ya bakteria kwenye mirija yako ya uzazi. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na pangusa (chlamydia) husababisha matukio mengi. Dawa za asili zenye Antibiotic zinaondoa kabisa tatizo hili.

Hali ya kuvimba kwa mirija ya uzazi inaambatana na PID na mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa, kama vile pangusa (chlamydia) na kisonono.

Lakini kumbuka ugonjwa huu ukiachwa bila kutibiwa, unaweza kusababisha uharibifu wa kudumu kwenye mirija ya uzazi na kusababisha ugumba kwako.

Uvimbe Wa Mrija Wa Uzazi Wa Muda Mfupi Au Mrefu.

Hali ya kuvimba kwa mrija wa uzazi inaweza kupimwa kama ya muda mfupi au mrefu.

Mrija wa uzazi unaovimba kwa muda huo huo huwa ni maambukizi kwenye mrija au mirija ya uzazi. Inatokea wakati mirija ya uzazi inapovimba na kutengeneza majimaji, na kusababisha kuta za ndani kushikamana na tishu zingine zilizo karibu. Mrija mmoja au yote miwili inaweza kujaa usaha.  Mirija hii inaweza kupasuka na kusababisha maambukizi makali kwenye nyonga.

Hali ya kuvimba kwa mrija ya muda mrefu huwa ni mbaya, ambayo hudumu baada ya mrija kuvimba kwa muda mfupi. Kwa kawaida hudumu kwa muda mrefu lakini hutoa dalili chache sana.

Hata hivyo, visababishi vya kawaida huwa ni maambukizi ya bakteria yanayosababishwa na magonjwa ya zinaa.

Pangusa (chlamydia) na kisonono ni magonjwa yanayoenea kwa urahisi sana kwa njia ya kujamiiana, na hivyo mara nyingi yenyewe hujitokeza bila dalili. Kwa sababu hii, kuvimba kwa mirija ya uzazi (salpingitis) huwa ni madhara mabaya sana kwa wanawake wenye umri wa miaka 16-25. Ni ugonjwa ambao huathiri karibia asilimia 12% ya wanawake kabla ya umri wa miaka 20.

Je, Dalili Za Kuvimba Kwa Mirija Ya Uzazi Zinakuwaje?

Mara nyingi, matatizo ya kuvimba kwa mrija (salpingitis) huwa hayana dalili. Madaktari wanaweza kuyatambua matatizo hayo wakati wanapofanya uchunguzi kwa kufanya vipimo kwenye maeneo ya nyonga. Dalili zinapoonekana, kwa kawaida huanza baada ya kumaliza kipindi cha hedhi, na zinaweza kuwa pamoja na:

  • Maumivu kwenye nyonga hasa wakati unapokuwa kwenye siku za hatari
  • Maumivu ya tumbo la chini
  • Tumbo kuunguruma
  • Mabadiriko ya rangi kwenye uteute unaotoka ukeni
  • Maumivu ya kiuno
  • Homa
  • Kichefuchefu au kutapika
  • Maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa
  • Kukojoa mara kwa mara

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Ikiwa ugonjwa huu utaachwa bila kutibiwa, basi hali ya kuvimba kwa mrija wa uzazi (salpingitis) inaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya kama vile:

  • Maumivu makali kwenye nyonga
  • Maumivu makali kwenye tumbo la chini
  • Maambukizi kuenea kwenye maeneo mengine kama vile, ovari, tumbo la uzazi(uterus) na maeneo mengine ya viungo vya uzazi
  • Kuwa mgumba kabisa

Pia unaweza kupata maelezo mengine kupitia link hizi hapo:

Fahamu Madhara 6 Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanamke.

Haya Ndio Madhara Ya Maambukizi Ya PID

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa za asili zenye uwezo mkubwa wa kutibu na kuondoa madhara ya kuvimba kwa mirija ya uzazi.

Unahitaji huduma, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Unataka kuungana na darasa letu la masomo ya afya, bonyeza link hii: wa.me/255752389252

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!