Mambo 8 Yanayosababisha Mlango Wa Kizazi Kuvimba.

Je, Kuvimba Kwa Shingo Ya Kizazi Maana Yake Ni Nini?

Kuvimba kwa shingo ya kizazi ni kutuna kwa mlango wa kizazi(cervicitis). Hali hii inapojitokeza huambatana na kutokwa na uchafu mwingi ukeni, kutokwa na damu damu au kuhisi maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndao, ingawa baadhi ya wanawake wanaweza wasihisi dalili zozote hata kidogo.

Wanawake wanaweza kuwa na uvimbe wa muda tu(ambao mar azote husababishwa na maambukizi) au uvimbe sugu(ambao nao mara nyingi husababishwa na muwasho).

Wanawake wanaweza kuwa na uvimbe wa muda tu(ambao mar azote husababishwa na maambukizi) au uvimbe sugu(ambao nao mara nyingi husababishwa na muwasho).

Je, Kuvimba Kwa Shingo Ya Kizazi Kunaathiri Nini?

Watu wenye wapenzi wengi wenye tabia ya kupenda ngono sana wapo katika hatari ya kupatwa na tatizo la kuvimba kwa shingo ya kizazi. Wale wenye historia ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, au wenye wapenzi wenye historia ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa wanaweza kupatwa na tatizo la kuvimba kwa shingo ya kizazi. Ugonjwa huu unaweza kusababishwa pia na muwasho kutokana na pedi kukaa ukeni kwa muda mrefu, kutawaza uke kwa kutumia sabubi au vitu vyenye marashi makali sana.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Je, Utajuaje Kama Shingo Ya Kizazi Imevimba?

Njia pekee ya uhakika ili kujua kama shingo ya kizazi imevimba ni kufanya kipimo tu hospitalini. Dalili za kuvimba kwa shingo ya kizazi utakazoziona ni pamoja na:

  • Kutokwa uchafu ukeni usio wa kawaida ambao unaweza kuwa wa njano, mweupe au kijivu na wenye harufu mbaya.
  • Kutokwa na damu ukeni pasipokutarajia
  • Maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa
  • Mahavu au uke kuwasha sana

Ni vyema kutafuta tiba haraka sana kama ukiona dalili yoyote kati ya nilizotaja hapo juu au kama uliwa kuwa na magonjwa ya zinaa hapo awali. Inapaswa pia ifahamike kwamba baadhi ya wanawake huwa hawaoni dalili za kuvimba kwa shingo ya kizazi. Kwahiyo, vipimo vya mara kwa mara ni vya muhimu sana ili kwamba daktari wake aweze kuona ikiwa kama kuna utofauti wowote kwenye kizazi chako.

Je, Shingo Ya Kizazi Inaweza Kuvimba Bila Maambukizi Ya Magonjwa Ya Zinaa?

Ndiyo. Kuvimba kwa shingo ya kizazi mara nyingi hakusababishwi na magonjwa ya zinaa. Wakati mwingine husababishwa na bakteria, aleji au majeraha.

Je, Visababishi Vyake Ni Nini?

Maambukizi ndio sababu kuu kwanini wanawake hupatwa na hali ya kuvimba kwa shingo ya kizazi kwa muda mfupi. Madhara yanaweza kutokea pale bakteria wanapoingia ndani kwenye mfuko wa uzazi. Visababishi vya kawaida kabisa vya kuvimba kwa shingo ya kizazi ni pamoja na:

  • Pangusa (chlamydia)
  • Kisonono (gonorrhea)
  • Mkanda wa jeshi
  • Malengelenge (Trichomoniasis)
  • Mycoplasma genitalium (ugonjwa mpya wa zinaa)

Vyanzo vya uvimbe wa shingo ya kizazi usiosababishwa na maambukizi hutokana na kemikali au muwasho. Hii ni pamoja na:

  • Muwasho utokanao na madawa ya kupulizia wadudu au matumizi ya kondom
  • Aleji ya pedi
  • Tiba ya mionzi au magonjwa ya uvimbe.

Je, Uvimbe Wa Shingo Ya Kizazi Unaambukiza?

Ndiyo. Maambukizi yanaweza kupita kwa mwenzi wako wakati mnaposhiriki tendo la ndoa. Kama umeshapimwa na ukakutwa na kuvimba kwa shingo ya kizazi, basi usishiriki tendo la ndoa angalau kwa siku 7 baada ya kupata matibabu na ikiwa kama dalili zimetoweka kabisa.

Je, Uvimbe Wa Shingo Ya Kizazi Unapimwaje?

Uvimbe wa shingo ya kizazi unaweza kupimwa wakati unapopima nyonga yote. Kipimo cha Pap smear kinaweza pia kutumiwa. Vipimo hivi humsaidia daktari wako kutambua seli za shingo yako ya kizazi pamoja na mfuko wa uzazi(uterus) kuwa hazipo katika hali ya kawaida. Daktari wako pia atachukua sampuli ya uchafu wowote ukeni ili kupima maambukizi kama vile kisonono, pangusa, malengelenge na bakteria ukeni. Wanapopangiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi Zaidi, basi daktari wako atachunguza vitu hivi vifuatavyo:

  • Wekundu wowote kwenye shingo yako ya kizazi
  • Uchafu unaotoka ukeni
  • Damu ukeni mwako au kwenye shingo ya kizazi
  • Kuvimba kwa kuta za uke.

Je, Uvimbe Wa Shingo Ya Kizazi Unatibiwaje?

Matibabu ya uvimbe wa shingo ya kizazi mara nyingi huwa ni ya antibiotic ili kuondoa maambukizi yoyote ya bakteria ambao wanaweza kusababisha uvimbe. Wanawake wenye umri chini ya miaka 25 au ambao wanajihusisha na tabia ya ngono wanapaswa kutibiwa kwa dawa za  antibiotic hata kama bakteria hawakupimwa. Baadhi ya bakteria wanaweza wasionekane kwa urahisi lakini bado wanaweza wakawepo.

Dawa za antibiotic za asili hutibu  uvimbe wa shingo ya kizazi.

Ndugu msomaji naomba niishie hapa, nipende kukaribisha kipindi cha maswali tu, karibuni sana.

Unaweza kutuma maoni yako, na pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuunganishwa na darasa letu uweze kujifunza zaidi juu ya mambo ya afya.

Je, Unahitaji huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252/0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *