MADHARA 3 YA KUVIMBA KWA KORODANI(ORCHITIS)

Nini Maana Ya Kuvimba Kwa Korodani(Orchitis)?

Orchitis ni kutuna au kuvimba kwa korodani moja au zote mbili. Korodani ni iungo vya mfumo wa uzazi wa mwanaume. Viungo hivi huzarisha mbegu na homoni za testosterone. Wanaume wote wana korodani mbili ambazo hukaa ndani ya kifuko kinachoitwa pumbu.

Je, Epididymo-orhitis Ni Nini?

Epididymo-orchitis ni kuwa na matatizo yote mawili kwa pamoja, yaani tatizo la kuvimba kwa korodani na kuvimba kwa mirija inayokuwa nyuma ya korodani inayobeba mbegu za mwanaume na kuzihifadhi kwenye korodani. Mirija ya korodani hutuna na kuvimba na hivyo kusababisha korodani kuuma.

Je, Nini Husababisha Kuvimba Kwa Korodani?

Kuvimba kwa korodani huendelea kwasababu ya maambukizi ya bakteria au virusi. Vyanzo vingi vya kuvimba kwa korodani hutokea kwasababu ya maambukizi katika njia ya mkojo yaani UTI, au magonjwa ya zinaa kama vile pangusa(chlamydia), kisonono au kaswende.

Kuwapo kwa kuvimba kwa mrija wa korodani kunaweza kusababisha korodani kuvimba.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kuvimba kwa korodani husababisha maumivu makali kidogo kwenye korodani na kutuna. Ugonjwa mara nyingi huanza kwenye korodani moja. Lakini unaweza kuenea kwenye korodani nyingine au kuathiri pumbu.

Dalili zingine za kuvimba kwa korodani huwa kama hizi zifuatazo:

  • Kuhisi uchovu
  • Homan a baridi
  • Msuli kuuma
  • Kichwa kuuma
  • Kuhisi kichefuchefu
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio.

Je, Hali Ya Kuvimba Kwa Korodani Inapimwaje?

Muuguzi wako atakufanyia vipimo ili kuchunguza korodani zilizovimba. Unaweza pia kufanyiwa vipimo hivi:

  • Vipimo vya damu, mkojo ili kuchunguza maambukizi ya bakteria au virusi, ikiwa pamoja na magonjwa ya zinaa.
  • Kipimo cha Ultrasonography ili kupima mtiririko wa damu kwenye korodani. Kipimo hiki husaidia kugundua msokoto wa mishipa ya korodani, hali ambayo hujitokeza na kuzuia mtiririko wa damu kwenda kwenye korodani.

Je, Nini Madhara Ya Kuvimba Kwa Korodani?

Kuvimba kwa korodani baada ya kubarehe hali ambayo huathiri korodani zote mbili kunaweza kupunguza kiwango cha mbegu za kiume na hivyo kuzifanya kuwa nyepesi. Ni mara chahche sana kuvimba kwa korodani humfanya mwaname kuwa tasa. Hali ya kuvimba kwa korodani haiathiri uzarishaji wa homoni za testosterone.

Kuvimba kwa korodani pia kunaweza kusababisha:

  • Mkusanyiko wa usaha kwenye korodani
  • Mkusanyiko wa majimaji kwenye korodani
  • Korodani kusinyaa

Makala yetu inaishia hapa, napenda nikaribishe kindi cha maswali na maoni yako.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kujiunga na darasa letu uweze kujifunza zaidi juu ya afya.

Unahitaji huduma, basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252/0712181626.

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *