Fahamu Mambo Yanayopelekea Mlango Wa Kizazi Kuvimba

Na ieleweke kuwa mlango wa kizazi ni sehemu ya chini ya mfuko wa kizazi(uterus). Na huu ndio mlango ambapo damu ya hedhi hupitia kutoka kwenye mfuko wa kizazi(uterus). Wakati wa kujifungua mtoto, mlango wa kizazi hutanuka ili kuruhusu mtoto apite.

Lakini kama ilivyo tishu yoyote ndani ya mwili, hivyo, mlango wa kizazi unaweza kuvimba kutokana na sababu mbalimbali. Hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi kitaalam huitwa, “Cervicitis”.

Miongoni mwa dalili ambazo wanawake wengi huzipata ni kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi na mabadiriko ya kutokwa na uchafu ukeni.

Je, Nini Husababisha Kuvimba Kwa Mlango Wa Kizazi?

Chanzo kikubwa cha kuvimba kwa mlango wa kizazi ni maambukizi. Maambukizi yanayosababisha mlango kuvimba yanaweza kuenezwa kutokana na mambo ya ngono, lakini pia zipo sababu zingine. Hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi inaweza kuwa ya kawaida au ikawa sugu. Uvimbe sugu wa mlango wa kizazi unaweza kuendelea kwa muda wa miezi kadhaa.

Hali ya uvimbe mbaya wa mlango wa kizazi husababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile:

  • Pangusa(Chlamydia)
  • Malengelenge(trichomoniasis)
  • Kisonono(gonorrhea)

Lakini pia hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi unaweza kusababishwa na maambukizi mbalimbali kama vile:

  • Matumizi ya sababuni au vipodozi vyenye marashi makali ukeni
  • Bakteria wa kawaida ukeni kama vile fangasi
  • Kemikali zinazokuwa kwenye ped
  • Mizio au aleji kutokana na kupasuka kwa kondom na hivyo kushindwa kutoka nje ya uke

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Mara nyingi kuvimba kwa mlango wa kizazi kunaweza kusionyeshe dalili, na unaweza  kujifunza kuwa una hali ya uvimbe huu baada tu ya kujaribu kuweka ped. Ikiwa kama kuna dalili zozote, basi zinaweza kuwa kama hizi zifuatavyo:

  • Kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu kuliko kawaida
  • Maumivu makali ukeni
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
  • Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa ambayo sio ya hedhi.
  • Maumivu ya mgongo
  • Kutokwa na uchafu mwingi ukeni wenye rangi ya njano au ukijani pamoja na usaha ukiambatana na harufu mbaya.

Mlango wa kizazi unaweza kuvimba ikiwa kama hali ya uvimbe itaendelea. Uchafu utokao ukeni wenye muonekano kama usaha ndio dalili za uvimbe mkubwa wa mlango wa kizazi.

Je, Nini Madhara Ya Kuvimba Kwa Mlango Wa Kizazi?

Hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi iliyosababishwa na kisonono, au pangusa(Chlamydia) inaweza ikaendelea kuharibu kuanzia ukuta wa mfuko wa kizazi mpaka kwenye mirija ya uzazi, na kusababisha ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi yaani PID (Pelvic Inflammatory Disease). Tatizo la maambukizi katika via vya uzazi au PID husababisha maumivu ya nyonga, kutokwa na uchafu, pia kupatwa na homa. Kumbuka tatizo la PID lisipotibiwa husababisha mwanamke kuwa mgumba.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo na madhara ya kuvimba kwa mlango wa kizazi. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Je, Unataka Huduma? Basi, walisiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *