JE, NINI KINACHOSABABISHA TITI KUVIMBA? JE, NINI DALILI NA MADHARA YAKE?

Na ieleweke kuwa, kuvimba kwa titi huwa ni kuathirika kwa tishu yake ambayo hupelekea titi kuuma, kuvimba, kuwa lenye unyevunyevu na hatimaye kuwa lenye rangi nyekundu. Hali hii pia inaweza kukusabbisha ukapatwa na homa au baridi kali. Kuvimba kwa titi mara nyingi huwaathiri wanawake wanaonyonyesha, ingawa wakati mwingine hali hii inaweza kutokea kwa wanawake ambao hawanyonyeshi.

680+ Mastitis Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images - iStock | Cow  mastitis

NUKUU: Hali ya kuvimba kwa titi kwa mwanamke anayenyonyesha hujitokeza ndani ya wiki sita za mwanzoni baada ya kujifungua mtoto, lakini ni hali ambayo inaweza kujitokeza baadaye wakati mwanamke anapokuwa akinyonyesha. Hali hii inaweza kumsababishia mama kujihisi mwili kunyong’onyea, na kumfanya ashindwe kumtunza mwanae.

Wakati mwingine hali ya kuvimba kwa titi inaweza kumsababisha mama akamuachisha mtoto wake kabla ya muda wake, lakini ataendelea kumnyonyesha tu hata kama akiwa natumia madawa kwa ajili kutibu tatizo lake.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Inapotokea hali ya kuvimba kwa titi, dalili zake huwa kama ifuatavyo:

  • Titi kuwa laini au unapoligusa linakuwa lenye unyevunyevu
  • Mara nyingi kujihisi kama kuumwa
  • Titi kuvimba
  • Maumivu au kuhisi kama moto muda wote au anaponyonyesha
  • Ngozi ya titi kuwa nyekundu
  • Homa kupanda juu

NUKUU: Ingawa hali ya kuvimba kwa titi mara nyingi hujitokeza katika wiki kadhaa za mwanzo za mama napoanza kunyonyesha, basi inaweza kujitokeza tena muda wowote wakati wa kipindi cha kunyonyesha. Hali ya kuvimba kwa titi inaweza kuathiri titi moja tu.

Je, Nini Kinachoweza Kukufanya Umuone Daktari Mapema?

Kwa kawaida utajisikia dalili kama vile mafua kwa masaa kadhaa kabla hujatambua kuwa titi lako lina eneo lenye rangi ya wekundu. Mara utakapogundua hali hii ya mchanganyiko wa dalili na ishara mbalimbali, basi bila shaka ndio muda wa kuanza utaratibu wa kumuona daktari hospitali mapema ili kufanya vipimo.

Je, Nini Kinasababisha Hali Ya Titi Kuvimba?

Na ieleweke kuwa, kazi ya kunyonyesha mtoto inahitaji ungalifu mkubwa mno na ndio maana baadhi ya wanawake wanaposhindwa kujali, ndipo hujitokeza hali ya titi kuvimba.  Visababishi vingine ni kama ifuatavyo:

  • Mrija wa titi unaotoa maziwa kuziba
  • Bakteria kuingia kwenye titi la mama

Je, Nini Madhara Yake?

Ikiwa kama titi halijatibiwa kabisa, au endapo kama mrija wa maziwa kwenye titi umeziba, basi kunaweza kukusanyika usaha na kulifanya titi kuendelea kuvimba na kusababisha eneo kama jipu gumu. Jipu mara nyingi huhitaji kupasuliwa ili kuondoa huo usaha. Kwahiyo, ili kuepukana na hali hii, yafaa sana ukamweleaza daktari wako mapema kadiri dalili au ishara zinapozidi kuendelea kujitokeza.

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo la kuvimba kwa matiti. Unahitaji kupata huduma hii, wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252/0712181626.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uunganishwe kwenye GROUP letu ujifunze masomo ya afya bure.

Karibu sana!

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *