JE, NI KAWAIDA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI? HEBU SOMA MAKALA HII!

Uchafu unaotoka ukeni huwa ni kitu kingine zaidi ya mzunguko wa hedhi, ambao wanawake huuona na kuanza kujiuliza ni kitu gani kinasababisha katika miili yao. Kama mizunguko yako ya hedhi sio ya kubadirika na inakuja kwa muda muafaka, na uchafu unaotoka ukeni ni wa kawaida, basi bila shaka utajisikia mwili wako kuwa ni wenye afya kabisa.

15 Examples of What to Say When a Woman Asks You a Challenging Question |  The Modern Man

NUKUU: Lakini kama mwanamke akianza kuona siku zake za hedhi zinaanza kuruka au kupata vipindi vya hedhi vingi na kutokwa na damu nyingi, basi wakati mwingine atafahamu tu kuwa mwili wake haupo vizuri.

Bado, wanawake wengi wamekuwa wakipata siku za hedhi na wanakuja kutambua kuwa uchafu unaotoka ukeni sio wa kawaida tena una harufu mbaya. Lakini jambo la kushangaza ni hili, muda wote mwanamke pamoja na mpenzi wake wataona ni jambo la kawaida  mwanamke kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya kama samaki aliyeoza.

How to Deal With Vaginal Odor

NUKUU: Wanawake hushindwa kufahamu nini cha kufanya. Inaaibisha muda mwingine mwanamke anapokuwa na hali kama hiyo ya kutokwa na harufu mbaya ukeni. Anaweza akawa najitawaza mara tatu kila siku, na bado atakuwa na hofu tu kwamba huenda harufu inayotoka ukeni bado inasikika kwa watu anaokuwa karibu naye. Ni vigumu sana kuiondoa harufu hiyo kwa kujitawaza tu, na bado utazidi kuwa na hofu kuwa mpenzi wako ataihisi harufu hiyo pale unapoenda kufanya naye tendo la ndoa.  Lakini marashi au sabuni za kuoshea maeneo hayo havitasaidia.

 

Ni pende kusema hivi,  ni jambo la kawaida  kutokwa na uchafu ukeni. Baadhi ya wanawake hutokwa na uchafu mwingi sana kuliko wengine , na hii ni kwasababu ya homoni kutokuwa katika uwiano sawa. Mabinti pamoja na wanawake wajawazito wote huwa na viwango vya juu sana vya homoni kuliko kawaida ambavyo husababisha muongezeko wa kutokwa na uchafu mwingi ukeni.

Now we know dangers of mesh implants... but are the alternatives to treat  incontinence any safer? | Daily Mail Online

NUKUU: Uchafu unaotoka ukeni ni wa muhimu sana katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Ute unaotengenezwa na tezi ndani ya uke na shingo ya uzazi huondoa seli zote zilizokufa pamoja na bakteria. Hii ndio huufanya uke uwe safi na husaidia kuzuia maambukizi. Badiriko kwenye uchafu wa kawaida ukeni yaweza kuwa ni dalili ya maambukizi ukeni.

Siku zote uchafu unaotoka ukeni huwa ni wa kawaida kabisa. Kiwango kinaweza kubadirika, na harufu pia, na rangi inaweza kuwa ya maziwa maziwa nyeupe, kutegemeana na muda wa mzunguko wako wa hedhi.

Mambo ya muhimu kuyachunguza ili kubaini kuwa kama kuna maambukizi pamoja na muda mrefu uliokuwa  ukitokwa na uchafu mbaya, rangi au harufu ya uchafu na uwepo wa muwasho wowowte, maumivu, hali ya kuwaka moto ndani au pembeni mwa uke.

Maambukizi mbalimbali huonekana na aina tofauti za uchafu na dalili, kwa mfano;

 

  1. Pangusa Na Kisonono

 

Maambukizi haya yapo wazi sana, kadiri kunapozidi kuwapo na kiwango kikubwa cha uchafu wenye rangi ya kijivu, njano, wenye harufu mbaya ambayo sio ya kawaida kabisa ukilinganisha na uchafu uanaotakiwa kutoka kila siku. Kwa nyongeza, inaweza kusababisha kukojoa mara kwa mara, kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu makali ya nyonga, kutokwa na damu, na mzunguko wa hedhi kubadirika badirika ikiwa kama halitatibiwa mapema.

Vaginal pain: Causes, symptoms, and treatment

Pia zaweza kuwa visababishi vya maambukizi katika via vya uzazi(Pelvic Infalammatory Diseases au PID) ambayo inaweza kusababisha maradhi makubwa, homa, kuziba kwa mirija, na hatimaye kupelekea hali ya ugumba.

  1. Malengelenge

 

Haya huwa ni maambukizi yatokanayo na vimelea hasa huambukizwa na kusababishwa na kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga, pale mwanamke anapotokwa na uchafu mbaya ukeni wenye rangi ya kijivu.

 

  1. Maambukizi Ya Fangasi Uken

 

 

Maambukizi ya fangasi yanaweza kuwa na aina mbili za uchafu, waweza kuwa uchafu mzito au wenye kuganda kama maziwa ya mgano au mwepesi, mweupe ambao husababisha muwasho mkubwa na uvimbe kwenye mashavu ya uke.

 

Baadhi ya wanawake hupenda kutumia kupaka madawa ukeni kama vile cream, nk,  lakini  kuna baadhi ya tiba zinazoweza kuzuia maambukizi ukeni ambayo yanaweza kupelekea kutokwa na uchafu mbaya;

 

  • Hakikisha eneo lako la uke nje linakuwa safi kwa kuliosha mara kwa mara kwa maji safi yakiwa ya vuguvugu. Usioshe ndani ya uke kwa kutumia sabuni. Kamwe usitumie sabuni zenye marashi, nk.

 

  • Baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa au kujisaidia kukojoa, hakikisha unasafisha uke kuanzia mbele kuelekea nyuma ili kuepusha maambukizi ya bakteria yasiingie ukeni. Tumia kitambaa kisafi au maji safi kuliko kutumia karatasi za chooni.

 

  • Mwisho kabisa jitahidi kuwa na mazoea ya kuvaa nguo za ndani zilizoshonwa kwa nyuzi za pamba, na uepuke nguo za ndani zenye kuba sana.

 

Napenda kuishia hapa ndugu msomaji. Je, unahitaji huduma kutoka James Herbal Clinic?

Tupigie kwa namba hii: 0752389252 au 0712181626.

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATSSAP tukaweza kukupatia link yetu uweze kujiunga na JAMES HERBAL GROUP ambalo ni darasa zuri linalotoa mafunzo mazuri ya afya kila siku katika mtandao wa TELEGRAM.

 

Karibuni sana.!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *