VIJUE VISABABISHI VYA MAUMIVU KWENYE NYONGA?

Je, Nini Maana Ya Maumivu Ya Nyonga?

 

Kama una maumivu maeneo ya chini ya tumbo lako au juu ya miguu yako, inahesabika kama maumivu ya nyonga. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo mengi sana. Inaweza kuwa dalili isiyokuwa na madhara kwamba una uwezo wa kubeba ujauzito, tatizo katika umeng’enyaji chakula, au ishara mbaya kiasi kwamba unahitaji kwenda hospitali haraka sana.

Back Pain Has A Real Foe: Radio Frequency Energy – National Pain ...

Unaweza ukaona hapo juu jinsi mtu mwenye tatizo hilo anavyokuwa.

 

 

  1. Kidole Tumbo

 

Kama ukiwa na maumivu makali eneo la kulia chini ya tumbo lako, kutapika, na ukahisi homa, basi inaweza kuwa ni tatizo la kidole tumbo. Kama ukiwa na dalili hizi, nenda katika chumba cha dharura.  Kidole tumbo kilchoambukizwa kinaweza kuhitaji upasuaji. Kama kikipasuka, kinaweza kueneza maambukizi ndani ya mwili wako.

How To Find The Appendix On Imaging - Stepwards

NUKUU: Hali hii inaweza kusababisha madhara makubwa mno.

 

  1. Kundi La Dalili Zinazojirudia Tumboni(IBS)

 

Je, unahisi maumivu makali tumboni, vichomi, tumbo kuunguruma, na kuharisha au kukosa choo dalili ambazo huendelea kujirudia mara kwa mara?  Ongea na daktari wako ili aweze kugundua tatizo. Yaweza kuwa tatizo liko tumboni. Lakini madaktari wengi huwa hawana uhakika nini kinachosababisha tatizo hili.Itchy Gut Nerves Responsible for Irritable Bowel SyndromeNUKUU: Ulaji, kutokuwa na msongo wa mawazo pamoja na tiba za asili vinaweza kusaidia kuondoa tatizo hili.

  1. Kuhisi Maumivu Wakati Yai Linapopevuka

 

 

Je, umewahi kuhisi maumivu makali kabla ya kipindi cha hedhi? Unaweza kuhisi mwili wako unapevusha yai. Unapopevusha yai, kifuko cha yai hutoa yai pamoja na uteute na damu. Hali hii inaweza kusababisha usumbufu. Hiyo ni kwasababu hutokea kila mwezi katikati ya  mzunguko wako wa hedhi. Maumivu yanaweza kuwa pembeni mwa tumbo la chini kila mwezi.

Painful Menstrual Periods: Causes, Treatments & MoreNUKUU: Huwa haina madhara sana na mara nyingi hutoweka yenyewe tu ndani ya masaa kadhaa.

 

  1. Maumivu Wakati Wa Tumbo La Hedhi

 

 

Mara nyingi unaweza kuhisi maumivu haya ndani ya tumbo lako la chini au mgongoni.Ni maumivu ambayo hudumu kwa muda wa siku 1-3. Kwanini yanakuwa maumivu? Kila mwezi, tumbo lako la uzazi hujenga ukuta laini wa tishu. Hapo ndipo kiini tete kinaweza kujipachika na kukua. Kama ukishindwa kubeba ujauzito, basi ukuta laini huo ndipo hupasuka na kubanduka wakati wa hedhi. Mfuko wa kizazi unapojikaza ili kutoa nje tishu laini ya ukuta huo, mwanamke huanza kuhisi maumivu na vichomi.

Abdominal cramps and vaginal discharge: Causes and treatmentNUKUU: Pia unaweza kuzungumza na daktari wako juu ya tatizo hili la maumivu wakati wa hedhi. Madawa fulani ya asili kutoka James Herbal Clinic yanaweza kukusaidia sana.

 

  1. Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi

 

 

Hali hii hutokea wakati kiini tete kinapojipachika mahali fulani nje ya mfuko wa kizazi na kuanza kukua. Hali hii mara nyingi hujitokeza kwenye mirija ya uzazi. Maumivu makali ya nyonga hasa upande mmoja, kutokwa na damu ukeni, pamoja na kuhisi kizunguzungu huwa ni dalili. Uonapo dalili hizi jitahidi kupata dawa haraka sana.

Ectopic Pregnancy: Symptoms, Causes, and TreatmentsNUKUU: Hii huwa ni hali inayotia hofu kwa muhusika.

 

  1. Maambuki Ya Magonjwa Ya Zinaa

 

Maumivu ya nyonga ni mojawapo ya ishara ya baadhi ya magonjwa ya zinaa. Magonjwa haya mawili huwa ni pangusa na kisonono. Mara nyingi unaweza ukapata maambukizi haya aina mbili kwa mara moja. Mara nyingi maambukizi haya huwa hayaonyeshi dalili.  Lakini pale dalili zake zinapojitokeza, unaweza kuhisi maumivu pale unapokojoa, kutokwa na damu ya hedhi mara 2 kwa mwezi, pia kutokwa na uchafu mbaya ukeni.

Egg White Cervical Mucus after Ovulation - Pregnant or Not?

NUKUU: Uonapo dalili hizi jitahidi kufika hospitali haraka sana. Pia ni vyema sana kupata vipimo pamoja na mwenzi wako na kufanya matibabu bila kuchelewa ili kuepusha maambukizi kwa wengine.

 

  1. Maambukizi Katika Via Vya Uzazi(PID)

 

Haya huwa ni madhara ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hii huwa ni chanzo kikubwa cha ugumba kwa mwanamke. Hali hii inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu kwenye mfuko wa kizazi, vifuko vya mayai, pamoja na mirija ya uzazi. Maumivu ya tumbo, homa, kutokwa na uchafu mbaya ukeni, na maumivu wakati wa tendo la ndoa au wakati wa kukojoa kunaweza kuwa ndio dalili.

Cramps after sex: Possible causes in men and womenNUKUU: Pata matibabu mapema ili kuzia maangamizi na madhara katika mfumo wa uzazi wako. Pia uanzapo kupata matibabu jitahidi kutibu pamoja na mwenzi wako.

 

  1. Vivimbe Katika Vifuko Vya Mayai

 

 

Vifuko vya mayai hutoa mayai pale mwili wako unapopevusha. Wakati mwingine kifuko cha majimaji kwenye mfuko wa yai huwa hakifunguki ili kuachia yai liweze kutoka nje. Au kinaweza kujifunga tena baada ya kufunguka na kujaa uteute. Hii husababisha uvimbe kwenye vifuko vya mayai. Mara nyingi huwa havina madhara kwani hutoweka vyenyewe. Lakini vinaweza kusababisha maumivu ya nyonga,  shinikizo, kuvimba na kuunguruma kwa tumbo.

Yumurtalığın kistası ilə bağlı 13 sual | Gənc Ailə

NUKUU: Na kama kifuko cha yai kikipasuka au kujikunja, kinaweza kusababisha maumivu makali ya ghafla. Uonapo hivi jitahidi kufika hospitali haraka sana ili kufanya vipimo kupitia Ultrasound.

 

  1. Uvimbe Kwenye Tumbo La Uzazi

 

 

Vivimbe hivi huote nje au ndani ya ukuta wa tumbo la uzazi. Vivimbe vya fibroid ni vya kawaida sana kwa wanawake wanapokuwa katika umri wa miaka 30-40. Mara nyingi vimekuwa vikisababisha matatizo kwa wanawake. Lakini baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na tatizo la kujaa gesi tumboni, maumivu kiunoni, kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, maumivu wakati wa tendo la ndoa au tatizo la kushindwa kupata ujauzito.

A Visual Guide to Uterine Fibroids

NUKUU: Uonapo haya unatakiwa kujitahidi kufika hospitali mapema ili kupata vipimo uweze kuanza matibabu bila kuchelewa.

 

 

  1. Maumivu Makali Ya Tumbo

 

 

Kwa baadhi ya wanawake, huwa kuna tishu inayoota nje ya mfuko wa kizazi ambayo hufanana na tishu inayotanda ndani ya ukuta wa mfuko wa kizazi. Inaweza ikajitokeza kwenye vifuko vya mayai, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo mpana na mwembamba na maeneo mengine ya mwili. Inapokuwa ni kipindi chako cha hedhi, haya mabonge ya tishu huvunjika. Lakini tishu huwa hazina njia ya kupita ili kutoka mwilini. Kwakuwa hii huwa ni mara chache sana kuwa hatari katika maisha yako, inaweza kusababisha maumivu na kujenga majeraha ya tishu ambayo yanaweza kumfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito.

NUKUU: Zipo njia mbalimbali za matibabu.

 

  1. Maambukizi Katika Njia Ya Mkojo(UTI)

 

 

Je, unakojoa mara kwa mara au unahisi maumivu wakati unapokojoa? Au je, unahisi kama vile kibofu chako kimejaa? Yaweza kuwa ni maambukizi katika njia ya mkojo(UTI). Hali hii hutokea pale vimelea vinapoingia kwenye njia yako ya mkojo. Lakini vimelea hawa wanapoenea mpaka kwenye figo, vinaweza kusababisha uharibifu mbaya sana.

Can a Urinary Tract Infection Cause Lower Back Pain?

NUKUU: Dalili za maambukizi kwenye figo huwa ni kuhisi homa, kichefuchefu, kutapika, pamoja na maumivu upande mmoja wa kiuno chako.

  1. Mawe Ya Figo

 

Haya huwa mabonge ya chumvi pamoja na madini ambayo mwili wako hujaribu kuepukana nayo kwenye mkojo. Yanaweza kuwa madogo sana kama punje ya mchanga. Mkojo wako unaweza kubadirika na kuwa wenye rangi ya pinki au nyekundu kutokana na damu.

Kidney Stone Treatment in Nigeria | Royan Urology Center Lagos

NUKUU: Fika hospitali haraka kama ukifikiri kuwa una tatizo la mawe ya figo. Pia daktari atakushauri unywe maji mengi mara kwa mara ili kukusaidia mawe ya figo yaweze kutoka.

 

  1. Kuvimba Kwa Kibofu Cha Mkojo

 

 

Hali hii husababishwa na maumivu endelevu na hutokana na kuvimba kwa kibofu cha mkojo. Huwa ni hali ya kawaida kwa wanawake wenye umri wa miaka 30-40. Madaktari huwa hawana uhakika na chanzo chake. Watu wenye maumivu kali ya kibofu cha mkojo wanaweza kuhitaji kukojoa mara kwa mara ndani ya lisaa 1. Unaweza pia ukahisi presha katika eneo la kinena, maumivu unapokojoa, na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

 

  1. Kadiri unavyokuwa mkubwa, hali hii inaweza kutokea.

 

Kibofu chako au mfuko wa uzazi hushuka chini. Mara nyingi huwa sio tatizo kubwa sana, lakini linaweza likakunyima raha. Unaweza kujisikia kitu kinasukuma maeneo ya ukuta wa uke, au tumbo lako la chini linaweza kujisikia kama limejaa vile. Pia inaweza kukupatia hali ya kutojisikia raha hasa maeneo ya nyonga au kiunoni na kukufanya uhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa. Hivyo mazoezi maalumu kama vile ya ngonga yanatakiwa kufanywa

 

  1. Nyonga Kukaza

 

 

Tumeona mishipa ya damu inayokunjamana kwenye miguu. Hali hii muda mwingine inaweza kujitokeza kwenye nyonga pia. Wakati damu inapokuwa inaenda huko na huko kwenye mishipa ya damu, ndipo huanza kutuna na kusababisha maumivu makali. Hali hii hufahamika kama nyonga kukaza. Hii huwa ni hali ambayo ni ngumu kuipima. Inaonekana kuwa inaumiza sana wakati unapokaa au kusimama.

Pelvic Congestion Syndrome - Victorian VascularNUKUU: Kulala chini kunaweza kukufanya ujisikie vizuri. Lakini kwakuwa matibabu yake hayajafamika sana, basi unahitaji kuwa na ukaribu mkubwa sana na daktari wako ili ujifunze njia gani ya kufanya na ni kitu gani kinaweza kufanya mambo mazuri kwako.

 

  1. Tishu Nyembamba

 

 

Kama uliwahi kupata maambukizi au kufanyiwa upasuaji, basi unaweza kupata maumivu endelevu kutokana na hali hiyo. Mshikamano ni aina ya tishu nyembamba ndani ya mwili wako. Tishu hizi hujengeka kwenye viungo vya mwili ambavyo havihitaji kushikama au kuunganika.

 Lysis of Adhesion | Long Island Laparoscopic Doctors

NUKUU: Muunganiko wa tishu fulani tumboni mwako unaweza kusababisha maumivu pamoja na matatizo mengine, inategemea na sehemu yatakapokuwa. Kwa nanma hiyo, unaweza kuhitaji njia za upasuaji ili kuepukana nanvyo.

 

  1. Maumivu Kwenye Mashavu Ya Uke(Vulvodynia)

 

Je, mashavu ya uke yanauma wakati unapoondesha baiskeli au unapofanya tendo la ndao? Kama unahisi yanawaka moto, yanachomachoma, au kupumapuma pembeni mwa mlango wa uke, basi yaweza kuwa yana tatizo. Hisia zinaweza kuendelea au kurudi tena na kutoweka. Kabla hujapima tatizo hili, daktari wako ataswa achunguze visababishi vingine. Hali hii huwa haisababishwi na maambukizi. Matibabu yako yanahitaji dawa tu.

 

 

  1. Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa

 

 

Hali hii inaweza kusababishwa na mambo mengi. Mambo hayo mengi hutibiwa. Yaweza kuwa maambukizi katika uke, au unaweza ukawa unahitaji uteute mwingi maeneo hayo ya uke. Jina la kitaalamu la tatizo hili ni, “dyspareunia”. Wakati mwingine maumivu hutoweka baada ya tendo la ndoa.

 

  1. Maumivu Ya Nyonga Ya Muda Mrefu

 

Kama una maumivu yanayodumu kwa muda wa miezi 6, yanaonekana hayo kuwa sugu. Yanaweza kuwa ni mabaya kwasababu yanakukoseha usingizi, maisha mazuri au mahusiano mazuri. Muone daktari haraka sana uweze kupata vipimo. Hali hii inapotibiwa vizuri hutoweka kabisa. Wakati mwingine, hata baada ya kufanyiwa vipimo vingi, kisababishi cha maumivu ya nyonga hubaki kama siri. Lakini daktari wako bado anaweza kukusaidia kuweza kupata njia ya kutibu tatizo hilo.

 

 

Je, unahitaji huduma yetu? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252/0712 181 626.

 

Pia unaweza kutuma namba yako ya whatssap tukaweza kukupatia link yetu ukajiunga na darasa au group letu katika mtandao wa telegram.

 

 

Karibuni sana!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *