JE, NINI CHANZO CHA KUONGEZEKA KWA MAJIMAJI NDANI YA KONDO WAKATI WA UJAUZITO (POLYHYDRAMNIOS)? JE, NINI DALILI ZAKE?

 

Polyhydramnios ni tatizo ambalo hujitokeza wakati majimaji mengi yanapokusanyika ndani ya mfuko wa kizazi wakati wa ujauzito. Neno Polyhydramnios ni kinyume cha neno Oligohydramnios ambalo humaanisha kuwa kuna majimaji kidogo sana kwenye kondo la mwanamke wakati wa ujauzito.

 

Tokeo la picha la image of Polyhydramnios

NUKUU: Kwenye tatizo la Polyhydramnios, hukusanyika majimaji mengi kwenye mfuko wa uzazi (uterus)wakati wa ujauzito. Tatizo hili linapojitokeza likiwa dogo tu linaweza likatoweka lenyewe. Endapo likiwa kubwa basi, litahitaji huduma ya matibabu haraka sana.

Kwa upande mwingine, majimaji kuongezeka kunaweza kusilete madhara, lakini bado pia linaweza lifanya ujauzito ukawa na matatizo mengi.

 

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

 

Tatizo hili linapokuwa dogo linaweza lisionyesha dalili zozote. Ni sawa kwasababu tatizo la kuongezeka kwa majimaji kwenye kondo wakati wa ujauzito halijitokezi kwenye matatizo yoyote ya ujauzito. Tatizo hili linapokuwa kubwa linaweza kusababisha dalili zifuatazo:

 

  • Kushindwa kupumua

 

  • Miguu kuvimba

 

 

  • Uke kuvimba

 

  • Kushindwa kupata mkojo

 

 

  • Kukosa choo

 

  • Kiungulia

 

 

  • Tumbo kukaza

 

Dalili nilizozitaja hapo juu hutokana na kukua kwa mfuko wa uzazi na kutoa msukumo kama vile presha kwenye viungo vingine vya uzazi.

Daktari wako anaweza kuwa tayari kutambua dalili za kondo kujaa majimaji. Kama mfuko wako wa uzazi utakuwa mkubwa sana, (baada ya kufanya vipimo wiki mbili au wiki kadhaa mbele) au kama daktari wako ameona matatizo anayoyahisi mtoto tumboni kama vile mapigo ya moyo, basi inaonyesha kuwa utakuwa na tatizo la kujaa majimaji kwenye kondo lako la uzazi.

Hali ya kuongezeka majimaji kwenye kondo wakati wa ujauzito inaweza kutokea mapema ndani ya wiki 16 za ujauzito, lakini matatizo mengine hayatajitokeza mpaka baadaye kwenye ujauzito wako. Hali ya kujaa majimaji kwenye kondo inapojitokeza mapema inaonyesha  uwezekano mkubwa wa matatizo kwenye ujauzito.

 

 

Je, Nini Visababishi Vyake?

 

Baadhi ya visababishi vyake huwa kama ifuatavyo;

 

  1. Ulemavu

 

Wakati mwingine kondo kujaa maji huwa ni madhara ya ulemavu ambao huharibu uwezo wa mtoto kumeza. Mtoto anameza majimaji pale anapokuwa kwenye mji wa mimba na hivyo huyakojoa, na kukifanya kiwango cha majimaji kiwe katika uwiano mzuri.

Picha inayohusiana

Kama mtoto akishindwa kumeza kutokana na ulemavu wa kijinsia, basi majimaji hutengenezeka  ndani ya tumbo la uzazi na kumfanya mtoto kuwa mlemavu. Angalia picha kwa mfano huyo mtoto hapo juu jinsi kichwa chake kilivyo.

 

  1. Magonjwa Ya Kisukari Wakati Wa Ujauzito

 

 

Kupanda kwa kiwango cha sukari kwenye damu kunaweza kusababisha kuongezeka kwa uwezekano wa kujengeka kwa majimaji ndani ya mfuko wa uzazi wa mjamzito. Madhara haya yanaweza kujitokeza pale mama alikuwa na tatizo la kisukari kabla hajapata ujauzito au ugonjwa wa kisukari ulipompata wakati wa ujauzito.

Tokeo la picha la image of a pregnant woman with marternal diabetes

Unaweza ukaona hapo kwenye picha pia jinsi tatizo hili linavyokuwa kwa mjamzito mwenye kisukari

 

  1. Watoto Mapacha Kutokuwa Na Uwiano Sawa Wa Damu Tumboni

 

 

 

Ikiwa kama umebeba mimba ya mapacha wenye kufanyana, yawezekana kabisa kwamba ukawa na madhara kwa mtoto mmoja ambaye atakuwa akipata damu nyingi, na mwingine atakuwa akipata damu kidogo.

 

Picha inayohusiana

Unaweza ukaona hapo juu pia jinsi mapacha wanavyokuwa kwenye mfuko wa uzazi pale kunapokuwa na tatizo la majimaji kujaa kwenye mfuko wa uzazi.

 

 

Je, Nini Madhara Ya Kuwa Na Majimaji Mengi Kwenye Tumbo La Uzazi?

 

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa, majimaji yanapokuwa katika kiwango kidogo, kwa kawaida huwa hayasababsihi madhara yoyote. Lakini ikiwa kama majimaji yatakuwa mengi, huwa kuna vitarishi mbalimbali kama vile;

 

  • Kujifungua mtoto kabla ya muda wake

 

  • Mtoto kichwa kuwa kikubwa pale anapokuwa tumboni

 

 

  • Kondo kupasuka

 

  • Kitovu kutokeza nje ya uke kabla mama hajajifungua

 

 

  • Mtoto kukaa upande

 

  • Kuchelewa kujifungua

 

 

Je, Vipimo Vya Tatizo Hili Vinafanyikaje?

 

 

Kama daktari wako atahisi kuwa una tatozo hilo la kuongezeka kwa majimaji kwenye kondo la uzazi, baada ya kuona dalili zako au muonekano wa vipimo vya ultrasound, yeye atafanya vipimo vingine zaidi ili kupima na kukisia ni kiwango gani cha majimaji kilichomo ndani ya mfuko wa uzazi. Ikiwa kama una visababishi vingi, basi daktari wako anaweza pia kufanya vipimo vingine zaidi

 

Je, Matibabu Yake Yanakuwaje?

 

 

 

Matibabu yanategemeana na ukubwa wa tatizo na nini kilichosababisha. Majiamji kwenye kizazi yanapokuwa katika kiwango cha kati kwa kawaida huwa hayahitaji matibabu yoyote. Daktari atakusihi uwe unaenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kuhakiki kuwa tatizo lisiwe kubwa. Lakini unapaswa ujifungue mtoto mwenye afya  bila kuwa na matatizo yoyote.

Tokeo la picha la image of birth defect in the placenta

Tatizo la kujaa majimaji kwenye kizazi linaweza kutibiwa kwa kutoa majimaji hayo kuyanyonya kwa kutumia sindano kubwa. Njia hii inaweza kusababisha madhara, hivyo daktari atapendekeza tu kama hatari ya kuwa na majimaji mengi kwenye kizazi itakuwa kubwa kuliko madhara ya kunyonya majimaji kupitia sindano.

Tatizo hili pia linaweza kutibiwa kwa njia ya madawa ambayo hupunguza kiwango cha mkojo ambao mtoto hutoa. Vidonge hivi husaidia kuzuia madhara ya mtoto anayoweza kuyapata kwenye moyo, hivyo utahitaji kupata uchunguzi wa vipimo kila mara ili kulinda mwendo wa moyo wa mtoto. Ikiwa kama tatizo ni kubwa, basi daktari anaweza kuamua kwamba njia nzuri katika matibabu ni kufanya matibabu mapema, wiki 37, au kabla ya wiki hizo.

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626

 

 

Arusha-Mbauda

 

Karibuni sana.

 

One thought on “JE, NINI CHANZO CHA KUONGEZEKA KWA MAJIMAJI NDANI YA KONDO WAKATI WA UJAUZITO (POLYHYDRAMNIOS)? JE, NINI DALILI ZAKE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *