JE, PID INAWEZA KUFANYA MGONGO WAKO KUUMA?

Kuna magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kusababisha maumivu kwenye nyonga kwa wanawake. Endometriosis ni mfano mojawapo, na PID ndio unafuata.

Lakini kama dalili zako zitakuwa ni maumivu ambayo husambaa kuelekea juu, basi lazima utakuwa unajiuliza je, PID inaweza kufanya mgongo wako uwe na maumivu? Hebu ngoja tuangalie Makala hii.

Je, Maumivu Kwenye Nyonga Ni Nini?

Wanawake kuwa na afya njema kwenye nyonga zao ni jambo la muhimu mno na kuna maradhi mengi ambayo yanaweza kusababisha maambukizi ya PID pamoja na maumivu.

22,000+ Woman Back Pain Stock Photos, Pictures & Royalty ...

Ugonjwa wa PID ni maambukizi ya kawaida kwenye njia ya uzazi wa mwanamke. Ugonjwa huu unaweza kusababisha maambukizi madhara kwenye viungo hivi:

  • Mirija ya uzazi
  • Mfuko wa uzazi(uterus)
  • Vifuko vya mayai(ovaries)
  • Uke, na
  • Mlango au shingo ya kizazi(cervix)

Sifa ni pamoja na maumivu kwenye nyonga na tumbo la chini pamoja na tumbo la uzazi au shingo ya kizazi kuumia pale unapofanyiwa vipimo. Matukio ya ugonjwa wa PID kwakweli huongezeka.

Endometriosis ni ugonjwa mwingine wa kwenye nyonga, wakati mwingine hukosewa na kuonekana  ugonjwa wa PID, ambao unaweza kusababisha maumivu makali na tumbo kuunguruma. Hali hii pia ianweza kukufanya uhisi tumbo kujaa gesi, na kusababisha kukosa choo na kupelekea uhisi maumivu ukeni au kwenye kizazi chako wakati unaposhiriki tendo la ndoa.

Vivimbe maji vidogovidogo kwenye vifuko vya mayai, mfuko wa uzazi kuvimba na mambo mengine kwenye afya yako ya nyonga yanaweza kusababisha uvimbe na hivyo kuhisi maumivu makali. Pia kuna mifano ambapo daktari hutambua maumivu sugu yanayoingilia mara kwa mara, ambayo humaanisha kwamba ugonjowa mmoja au Zaidi husababisha maumivu. Kwa mfano mwanamke anaweza kuugua matatizo ya kuhara au kukosa choo mara kwa mara ikiwa pamoja na endometriosis.

Pia kuna ugonjwa unaojulikana kama, “crosstalk” yaani maumivu kwenye kiungo kwenye nyonga ambao unaweza kusababisha maumivu sugu. Hii ni pale kiungo kimoja husambaza ishara kwenye kiungo kingine, na kusababisha maumivu kwenye kiungo hicho au kupunguza utendaji kazi wake.

Je, Ugonjwa Wa PID Unaweza Kusababisha Mgongo Kuuma?

Ugonjwa wa PID mara nyingi huwa haunyeshi dalili, lakini unaweza kusababisha maumivu kwenye tumbo la chini na, unaweza kusababisha maumivu kwenye kiuno chako.

Hapo ndio hufanya kuwa vigumu kubaini hasa nini kibaya; maumivu kwenye nyonga yanaweza kuwa tofauti kutegemeana na chanzo chake. Yanaweza kuwa maumivu makali au kidogo; yanaweza kuwa endelevu au yanaweza kuja na yakatoweka tena; yanaweza kuwa ya kawaida, makali kidogo au mabaya Zaidi; unaweza kutambua maumivu tu katika muda Fulani, kama vile wakati unapoanza kushiriki tendo la ndoa. Na maumivu ya nyonga yanaweza kusambaa kwenye kiuno chako, matakoni au kwenye mapaja na kushuka chini miguuni. Naomba uwe makini sana ndugu mpendwa unayesumbuka na ugonjwa huu.

Maumivu kwenye nyonga yanaweza pia kuja ghafla, yanayofahamika kuwa maumivu makali au unaweza kuwa nayo kwa muda mrefu tu, ambayo hufahamika kama maumivu sugu ya nyonga. Hii kwakawaida ni maumivu ambayo yamekuwapo kwa muda wa miezi 6 au Zaidi.

Wanawake wanaoteseka na maumivu sugu ya nyonga sio wao tu. Hii aina ya maumivu sugu ya nyonga inaaminika kuwakilisha kati ya asilimia 14% na 24% ya wanawake wenye umri wa kuzaa, karibia asilimia 14% ya wanawake hupatwa na maumivu endelevu ya nyonga katika umri wao. Kama unaumwa mgongo, au kiuno inaweza kuwa ni matokeo ya ugonjwa wa PID.

Je, Unaeza Kufanyaje Kuhusu Maumivu Ya Mgongo?

Kama una maumivu ya nyonga ambayo yanaonekana kusambaa kwenye mgongo, basi fika hospitali. Kama una ugonjwa wa PID, basi hatimaye unaweza kuharibu maeneo ya mfumo wako wa uzazi. Yanaweza kuwa maumivu makali na ugonjwa huu unaweza kukufanya ushindwe kubeba ujauzito.

Ugonjwa wa PID unaweza pia kusababisha kuwa na vivimbe maji kwenye vifuko vya mayai na hivyo kukufanya uwe mgonjwa sana. Unapofahamu tatizo, basi matibabu yapo yanapatikana ili kukusiaida. Kwahiyo usipende kuficha ugonjwa.

Naomba makala yetu iishie hapa, nipende kuwakaribisha wapendwa wenye maswali na maoni yenu, karibuni sana.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kujiunga na darasa letu uzidi kujifunza zaidi mambo ya afya.

Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *