SABABU 12 ZA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAMKE (HORMONAL IMBALANCE)

Hali ya kutokuwa na uwiano sawa(hormonal imbalance) kwa wanawake hutokea pale vichocheo au homoni zinapopanda sana au kushuka sana na kufikia viwango vya chini kwenye mkondo wa damu. Vichocheo au homoni huwa ni kemikali zinazozarishwa na tezi katika mfumo wa endocrine zinazoambia seli, tishu, pamoja na viungo, kitu gani cha kufanya. Vichocheo(hormones) husaidia kurekebisha kazi nyingu muhimu katika mwili wako. Naomba ulifahamu hili wewe unayesoma makala hii!

Hormone Imbalance Images - Free Download on Freepik

 

Kazi muhimu za vichochezi au homoni huwa ni nyingi mno na kila mmoja anapaswa kuzielewa, nazo ni kama hizi zifuatazo:

  • Kutengeneza hali ya mwili
  • Kurekebisha joto la mwili
  • Kuyeyusha mafuta mwilini
  • Kurekebisha viwango vya moyo
  • Kutengeneza usingizi mnono
  • Kutengeneza mzunguko wa hedhi
  • Kumfanya mtu kukua vizuri
  • Kurekebisha msongo wa mawazo

Viwango vya homoni kwa wanawake kwa kawaida hubadirika kwa nyakati fulani, kama vile kabla au wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito au wakati wa kukoma hedhi.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Tumbo kujaa gesi, mwili kuwa mnene, uchovu wa mwili, kujisikia vibaya, mwili kutokwa na jasho ni baadhi ya dalili nyingi za homoni imbalansi kwa wanwake. Vipindi vya hedhi kuruka au kuchelewa vinaweza pia kusababishwa na homoni imbalansi. Uwiano huu unaweza kuathiri afya, utendaji wa kazi, mahusiano ya ndoa pamoja na faraja ya moyo wa muhusika. Dalili za homoni imbalansi kwa wanawake ni kama hizi zifuatazo:

  • Kutokwa na jasho wakati wa usiku
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa
  • Kutokushika ujauzito
  • Kuhisi kichefuchefu
  • Kukosa usingizi
  • Kuwa na huzuni
  • Kukosa hamu ya kula
  • Sauti kuwa nzito
  • Kubadirika kwa mapigo ya moyo
  • Matiti kuuma
  • Uso kuvimba
  • Kichwa kuuma
  • Ugumu wa kuzingatia
  • Mwili kujaa
  • Uzito kuwa mkubwa au
  • Uzito kupungua
  • Kuwa na harara kwenye ngozi
  • Ngozi kukauka
  • Uvimbe shingoni
  • Mifupa kudhoofika
  • Nywele kuwa nyembamba
  • Nywele kunyonyoka
  • Mabadiriko ya sukari kwenye damu
  • Kuhisi kiu
  • Matatizo ya macho
  • Kisimi cha uke kuwa kikubwa
  • Kuhisi uchovu sana

Je, Nini Husababisha Homoni Imbalansi?

Mara nyingi wanawake hupatwa na tatizo la homoni imbalansi katika maeneo yanayotabirika na yanayotekea kiasili katika maisha yao(wakati wa hedhi, kabla ya kuvunja ungo, au wakati wa  ujauzito na hedhi kukoma). Lakini bado vipo visababishi vingine kama vile matumizi ya madawa mbalimbali, tabia ya mitindo ya maisha, mazingira ya kuishi, na kutokufanya kazi kwa tezi ya endocrine yaweza kuwa visababishi vingine vya homoni imbalansi kwa wanawake.

Tezi za endocrine huwa ni seli zinazokuwa mwilini pote ambazo huzarisha, huhifadhi na kisha hutoa homoni kwenye mkondo wa damu. Tezi tofauti za endocrine hurekebisha viungo mbalimbali vya mwili.  Visababishi vya homoni imbalansi kwa wanawake ni pamoja na:

  • Vyakula visivyokuwa na virutubisho
  • Msongo mkubwa wa mawazo
  • Mafuta mengi mwilini
  • Uvimbe wa tezi ya pituitary
  • Kisukari aina ya kwanza nay a pili
  • Kuvimba kwa kongosho
  • Maambukizi sugu hasa PID
  • Tezi ya thyroid kufanya kazi sana au kushindwa kufanya kazi
  • Matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango
  • Utumiaji wa madawa ya kurekebisha homoni
  • Uvimbe ambao huathiri tezi ya endocrine
  • Kupigwa mionzi, nk

Je, Homoni Inapimwaje?

Unapofika hospitali, homoni imbalansi kwa kawaida inapimwa kwa vipimo mbalimbali. Daktari wako ataanza na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa mwili wako, atakuuliza dalili unazozipata, na anaweza kupendekeza ufanyiwe vipimo vifuatavyo:

  • Kipimo cha damu: Kipimo cha damu kinaweza kupima viwango vingi vya damu
  • Kipimo cha nyonga: Kipimo cha nyonga kinaweza kuonyesha uvimbe
  • Kipimo cha Ultrasound: Kipimo hiki hutumia mawimbi kushika sura ya tumbo la uzazi(uterus), vifuko vya mayai(ovaries), tezi ya thyroid na pituitary
  • Kipimo cha X-ray
  • Kipimo cha MRI

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Wanawake wengi wanaposhindwa kuondoa tatizo la kuvurugika kwa homoni, wanachoambulia huwa ni madhara uke kuwa mkavu, pia kutokupata ujauzito kabisa(ugumba).

Ndugu msomaji naomba niishie hapa katika makal yetu hii, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuunganishwa na darasa letu uweze kupata elimi zaidi ya afya.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kutatua tatizo hili na kukusaidia kupata ujauzito. Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252/0712181626,

Arusha-Sombetini, Mbauda.

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *