JE, JINSI GANI UVIMBE KWENYE MFUKO WA KIZAZI HUATHIRI UJAUZITO PAMOJA NA UWEZO WA KUPATA UJAUZITO?

Fibroids sio salatani bali ni vivimbe ambavyo huota ndani au nje ya mfuko wa kizazi(uterus) au mji wa mimba. Vivimbe vinaweza kushambulia ujauzito au kuondoa kabisa hali au uwezo wa kupata ujauzito.

540+ Uterine Fibroid Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images - iStock  | Uterus, Fibroids, Uterine fibroids

NUKUU: Vivimbe kwenye kifuko cha uzazi huwa ni vya kawaida kabisa. Tukiangalia asilimia 20%-80% ya wanawake wamekuwa wakipatwa na tatizo la uvimbe wanapofikia umri wa miaka 50, na asilimia 30% ya wanawake wenye umri kuanzia miaka 25 na 44 wamekuwa wakionekana na dalili za uvimbe wa fibroids. Hii inamaanisha kuwa uvimbe wa fibroid unaelekea kuwa wa kawaida sana kwa mwanamke anapofikia umri wa kuzaa.

Je, Nini Madhara Ya Uvimbe Wa Fibroid Kwa Mjamzito?

Wanawake wengi wanaweza wasione madhara ya uvimbe wa fibroid pale wanapokuwa wajawazito. Hata hivyo inaonyesha kuwa asilimia 10%-30% ya wanawake wenye uvimbe wa fibroids hupatwa na madhara wanapokuwa wajawazito. Madhara yanayowapata wajawazito wenye uvimbe wa fibroid huwa ni maumivu makali au kutokwa na damu nyingi tena kwa mfululizo.

Hali hii pia mara nyingi huonekana kwa wanawake wenye uvimbe mkubwa zaidi ya sentimita 5 ambao wenye ujauziti wa miezi 6.

Uvimbe wa fibroid unaweza kuongeza vihatarishi kwa madhara mengine wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Ihatarishi hivi huwa kama ifuatavyo:

  • Mtoto Kushindwa Kukua Tumboni: Uvimbe mkubwa wa fibroid unaweza kuzuia kiumbe tumboni kisikue kutokana na kupungua kwa nafasi kwenye mji wa mimba.
  • Kubanduka Kwa Kondo(Placental Abruption): Hali hii hutokea wakati kondo linapobanduka kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi kwasababu limezibwa na uvimbe wa fibroid. Hali hii hupunguza hewa ya oksijeni pamoja na virutubishi.
  • Kuzaa Mtoto Kabla Ya Muda Wake: Maumivu yatokanayo na uvimbe wa fibroid yanaweza kusababisha mfuko ukafinyana hali ambayo inaweza kupelekea mama mjamzito kujifungua mtoto kabla ya muda wake.
  • Mimba Kuporomoka: Utafiti unaonyesha kuwa nafasi ya mimba kutoka ika mara dufu zaidi kwa wanawake wenye uvimbe wa fibroid.
Je, Nini Madhara Ya Ujauizto Kwenye Vivimbe Vya Fibroids?

Ukubwa wa fibroid huwa haubadiriki katika ukubwa wake wakati mwanamke anapokuwa mjamzito, lakini baadhi ya vivimbe hupungua. Kusema kweli, 1/3 ya chanzo cha uvimbe wa fibroid unaweza kuota pale mwanamke anapokuwa na ujauzito wa mwezi 1-3. Ukuaji wa uvimbe huu huchochewa na homoni ya estrogen, na viwango vya homoni ya estrogen hupanda juu wakati wa ujauzito. Hali hii inaweza kusababisha uvimbe kuanza kuota.

Lakini bado pia kwa wanawake wengine, uvimbe unaweza ukasinyaa kabisa wakati wa ujauzito. Katika utafiti inaonyesha kuwa alilimia 79% ya uvimbe ambao uliokuwepo hapo awali kabla ya kupata uajuzito hupungua ukubwa wake baada ya kujifungua.

Je, Nini Madhara Ya Uvimbe Kwenye Uzazi?

Wanawake wengi wenye uvimbe wa fibroid wanaweza kupata ujauzito vizuri kabisa. Matibabu na yanaweza yasiwe ya lazima sana. Kwa upande mwingine hata hivyo uvimbe wa fibroid unaweza kushambulia uwezo wa mwanamke kuzaa. Kwa mfano, uvimbe wa fibroid aina ya submucosal ambao huota na kupanuka kwenye kizazi, kwahiyo huongeza vihatarishi vya ugumba au kutokupata ujauzito kabisa.

Pamoja na kuwa uvimbe wa fibrois unaweza kusababisha hali ya ugumba kwa baadhi ya wanawake, lakini bado maelezo mengine ya ugumba yanaonyesha kuwa ya kawaida kabisa. Ikiwa kama una tatizo la kutokubeba ujauzito, daktari wako anaweza kukuelezea vyanzo vingine kabla hajakuambia habari ya uvimbe.

Je, Dalili Za Uvimbe Zinakuwaje?

Unaweza usiwe na dalili zozote za za fibroids. Kama huna dalili zozote, dalili kuu huwa ni zifuatavyo:

  • Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
  • Kutokwa na damu ya hedhi mara 2 kwa mwezi
  • Kutokwa na matone ya damu
  • Kupungukiwa na damu kutokana na kutokwa damu nyingi
  • Kutokwa na damu muda mrefu
  • Tumbo kujaa gesi
  • Kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
  • Maumivu ya kiuno
  • Kukosa choo
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kushindwa kumaliza mkojo kwenye kibofu.
  • Matatizo ya uzazi kama vile ugumba, mimba kuporomoka, au kuzaa kabla ya muda wake

Uvimbe wa fibroid unaweza kuuhisi wakati nyonga zinapopimwa. Ikiwa kama daktari wako atahisi kuwa una uvimbe, basi anaweza kuamua kutumia kipimo  kwa kuzamisha ndani ya uke, au kutumia ultrasound, ili kuhakiki ukuaji wa uvimbe huo kuwa ni wa fibroid na wala sio kitu kingine zaidi.

Je, Uvimbe Wa Fibroid Unatibiwaje Kabla Ya Kupata Ujauzito Ili Kuboresha Uwezo Wa Mwanamke Kupata Mimba?

Kutibu uvimbe kabla ya kupata ujauzito kunaweza kusaidia mwanamke akapata ujauzito. Matatibabu yanayotumika ili kuondoa tatizo hili huwa ni ya asili tu, nayo ni kupitia dawa nzuri kabisa kutoka JAMES HERBAL CLINIC.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuungana nasi katika GROUP au KUNDI la kujifunza masomo ya afya kila siku na utapata huduma.

Je, Unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Arusha-Mbauda,

 

Karibu sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *