JE, MBEGU ZA MWANAUME ZILIZO BORA NA ZENYE AFYA ZINAKUWA NA LADHA NA HARUFU GANI NA HUWA NA MUONEKANO GANI?

Baadhi ya watu wanaweza kujiuliza je, ladha ya manii au shahawa huwa ikoje, au harufu yake inakuwaje. Wakati unapoweza kubadirisha sifa hizi, basi mabadiriko yanaweza pia kuwa ishara ya matatizo.

Ladha, harufu, rangi na muonekano wa manii unaweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Manii zinaweza pia kubadirika kutoka kwenye kishindo kimoja kwenda kingine(yaani unapomwaga shahawa lile pigo la kwanza zinaweza kuwa na rangi yake na muonekano wake tofauti kabisa na pigo lingine litakalofuata). Mara nyingi, mabadiriko haya huwa ni ya kawaida, lakini baadhi yake yanaweza kuashiria huduma ya tiba.

24,600+ Male Infertility Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images -  iStock | Male fertility, Infertile man, Ivf

Shahawa zenye harufu mbaya baadhi ya maswali ya kawaida kuhusu jinsi mbegu zenye ubora zinavyopaswa kuwa na muonekano, harufu na ladha. Pia ziashiria mabadiriko ambapo uchunguzi na utafiti unapaswa kufanyika.

Makala hii inajibu baadhi ya maswali juu ya mbegu zenye ubora zinavyopaswa kuwa na muonekano, harufu na ladha yake.

Je, Manii Nini?

Manii zina rangi ya ukijivu, majimaji meupe yanayotoka kwenye uume unapofika kileleni. Haya majimaji yanakuwa na seli za mbegu(spermatozoa) na majimaji yenye kuvutika na kunata, kitaalamu tunaita “seminal fluid.”

Kazi ya majmaji ya manii ni kusafirisha mbegu(shahawa) na kuzipatia virutubishi na mazingira thabiti ili ziweze kuishi kwa muda wa siku tano hivi, ili kusaidia urutubishaji wa yai la mwanamke. Naomba ushikilie sana Makala hii wewe mwanaume unayesoma!

Katika kila kishindo, inaonyesha kuwa takribani seli za mbegu milioni 100 hutolewa kwenye uume.

Je, Manii Huzarishwaje?

Seli za mbegu huzarishwa kwenye korodani na baadaye husafisrishwa kwenye mrija mwembamba uliojikunjakunja. Hapo, mbegu hukomaa kwa uwezo wa homoni kutoka kwenye korodani na tezi ya pituitary. Mchakato huchukua takribani miezi miwili au mitatu.

Mbegu zinapokomaa, ndipo seli za mbegu huhamia kwenye mrija mrefu unaoitwa, “vas deferens” ambapo huchanganyikana na majimaji ya manii yaliyotengenezwa kupitia njia inayoitwa mrija wa kutolea shahawa pale unapofika kileleni. Uzarishaji wa mwisho huwa ni manii.

Majimaji ya manii yenyewe yamechanganyikana na uteute kutokana na viungo vitatu:

1.Tezi ya Cowper

Kiungo hiki chenye ukubwa wa peasi huzarisha uteute ambao hufanyakazi kama kilainishi na husaidia kupunguza asidi ili kuzifanya seli za mbegu ziweze kuishi.

2.Tezi Dume

Tezi hii yenye ukubwa wa karanga hutengeneza uteute ambao huzifanya manii ziwe katika muonekano wa majimaji wakati inatoa virutubishi na enzam ambavyo hurutubisha na kulinda seli za mbegu au shahawa.

3.Mirija Ya Manii

Hii huwa ni mirija miwili ambayo huzarisha majimaji yenye wingi wa fructose(sukari inayotumika kwa ajili ya mafuta) pamoja na prostaglandins(aina ya mafuta ambayo husababisha uke kujibinya ili kuzivuta shahawa zitoke kwenye uume kupitia mrija mrefu unaoitwa urethra(njia ya mkojo) na hivyo kuingi ukeni. Kwahiyo hii habari pia wanawake naomba muifahamu kwamba uke unapaswa kujibinya hasa unahisi kufika kileleni.

Je, Mbegu/Shahawa Zinadumu Muda Gani?

Kiwango cha mzunguko wa uhai wa mbegu za mwanaume huwa ni siku 74. Baada ya kufika kileleni, mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa muda wa siku tano.

Ladha Na Harufu Ya Shahawa

Shahawa zinaweza kuwa na ladha ya chumvichumvi, utamu Fulani hivi, au uchungu na zina harufu kali ya klorini sawa na mti wa peasi unaochanua. Shahawa kwa kawaida huwa ni chachu sana kuliko asidi, mazingira ambayo seli za manii hustawi. Uwiano wa joto bora kwenye manii huambatana na harufu kama ya chlorine hivi.

Sukari inapokuwa nyingi kwenye manii inaweza kuzifanya shahawa kuwa na ladha yenye utamu. Hata hivyo, hali ya alkaline inapokuwa kubwa kwenye manii inaweza kuzifanya shahawa kuwa na ladha ya chumvichumvi au uchungu kwa mbali.

Jinsi Gani Chakula Huathiri Harufu Na Ladha Ya Manii

Vyakula Fulani vinaweza kubadiri ladha na harufu ya manii, na kuzifanya kuwa na uchungu, na harufu kali. Hii ni pamoja na:

  • Pombe
  • Kabeji
  • Kahawa
  • Maziwa mgando
  • Kitunguu swaumu
  • Nyama
  • Kitunguu maji

Vyakula vingine vinasemekana kuwa vinaweza kuzifanya shahawa kuwa na ladha au harufu ya kawaida au yenye utamu, ni nanasi, mboga aina ya parsley, na celery.

Je, Lishe Inaweza Kuathiri Ubora Wa Manii Na Uzazi?

Tafiti zinaonyesha kile unachokula na kunywa kinaweza kubadiri ubora wa mbegu za mwanaume na uwezo wa kuzarisha mwanamke. Lishe yenye nyama nyingi zilizosindikwa, mafuta ya mgando pamoja na maziwa yaliyosindikwa yanaweza kuathiri umbo, ubora na mwendo wa mbegu za mwanaume. Vyakula vya samaki, matunda, mbogamboga, na karanga zinaonyesha kuwa na uwezo wa kuongeza ubora wa mbegu za mwanaume.

Mambo Mengine Matano Ambayo Yanaweza Kubadiri Manii

Kuvuta tumbaku kunaweza pia kubadiri ladha au harufu ya manii. Uvutaji sigara unaweza pia kupunguza ubora, kiwango, na mwendo wa mbegu za mwanaume na kukufanya wewe ushindwe kumpatia mwanamke ujauzito.

Mambo mengine ambayo yanaweza kuharibu ladha na harufu ya manii ni maambukizi. Hii ni pamoja na:

  • Maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)
  • Pangusa
  • Kisonono
  • Malengelenge

Harufu mbaya ya muozo au shombo la samaki inaweza kuwa ishara ya UTI au magonjwa ya zinaa, hasa ikiwa kama yakiambatana na kuvimba kwa korodani au kutokwa na uchafu usio wa kawaida kwenye uume. Mambo haya mawili yanaweza kuathiri uwezo wako wa kumpa mwanamke mimba ikiwa kama yakibaki bila kutibiwa. Kwahiyo fika hospitali haraka iwezekanavyo.

Je, Manii Zina Muonekano Gani

Manii za kawaida sio nyeupe sana wala za njano kwa mbali. Muonekano wake unapaswa kuwa sawa na ute wa yai la kuku. Wakati mwingine zinaweza kuwa nzito hivi kama una muda mrefu hujamwaga shahawa.

Mabadiriko kwenye rangi ya manii au muonekano huwa ni mdogo sana, lakini mabadiriko maalumu yanaweza kuhusiana na afya.

Mbegu Nyepesi

Mbegu za mwanaume wakati mwingine zinaweza kuwa nyepesi kama majimaji. Yaweza kuwa kwasababu umemaliza kufika kileleni na kupiga mshindo mmoja au miwiili kwa mfululizo, au mekunywa maji mengi, au korodani zako zimepatwa na joto kali kupita kiasi kutokana na kuvaa nguo za ndani za kubana sana na kufanya mazoezi ya nguvu nyingi. Kwa jambo kama hili, huo umajimaji unaweza kuwa wa kawaida tu na wala usikutishe ukawa na wasiwasi.

Mapungu Ya Madini Ya Zinki Pia Yanaweza Wakati Mwingine Kusababisha Mbegu Kuwa Nyepesi, Na Zenye Kuteleza.

Wakati mwingine, shahawa zenye majimaji zinaweza kuwa ishara ya mbegu kuwa chache(oligozoospermia). Hii hutokea pale kunapokuwa na mbegu chache kuliko mbegu milioni 15 kwa ujazo wa manii. Manii zenye majimaji ni tabia ya mbegu kuwa chache, ugonjwa unaoweza kusababishwa na:

  • Kuvimba kwa mishipa myembamba kwenye korodani
  • Maambukizi ya zinaa kama vile kisonono na pangusa
  • Kuvimba kwa korodani
  • Mbegu kutoka na kurudi ndani
  • Matatizo ya homoni
  • Saratani ya korodani

Shahawa Nyekundu Au Za Kahawia

Kama shahawa zako zina zina rangi ya wekundu au ukahawia Fulani, inaweza kuwa ishara ya damu. Pamoja na kwamba hii inaweza kuonekana ni tahadhari, basi kuwepo kwa damu kwenye shahawa inaweza kuwa sio tatizo sana. Mara nyingi husababishwa na mishipa midogo ya damu kupasuka kwenye mishipa ya manii au tezi dume wakati uume unapodindisha au unapomwaga mbegu.

Visababishi vingine vya kuwepo kwa damu kwenye shahawa ni pamoja na:

  • Tezi dume kuvimba
  • Kuvimba kwa mrija wa kusafirishia mbegu hasa kutokana na maambukizi
  • Kuvimba kwa korodani kutokana na maambukizi
  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
  • Matatizo ya figo au mawe kwenye figo

Habari njema ni kwamba matatizo mengi ya kuwepo kwa damu kwenye shahawa hutoweka yenyewe. Ni mara chache sana kuona kwamba kuwepo kwa damu kwenye shahawa ni dalili za saratani.

Shahawa Zenye rangi Ya Ukijani Au Njano

Shahawa zenye rangi ya ukijani au njano zinaweza kuwa ni dalili za maambukizi. Zipo sababu zingine ikiwa pamoja na:

  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono au malengelenge
  • Kuvimba kwa tezi dume mara nyingi kutokana na maambukizi
  • Manjano kutokana na homa ya ini
  • Kuwepo kwa mawe kwenye figo
  • Ugumba kutokana na wingi wa chembe hai nyeupe za damu ambazo huharibu na kudhoofisha seli za mbegu

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo wa kuondoa chanzo cha mbeguza mwanaume kuwa nyepesi, au kuwa na rangi au harufu mbaya kutokana na maambukizi, hivyo unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252/0712181626.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ukaweza kuungana nasi katika darasa au group letu ili uweze kujifunza zaidi juu ya magonjwa haya ya uzazi.

James Herbal Clinic tunapatika Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *